Maelekezo kwa
waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano, vyuo ufundi na chuo
cha 'manegement' na maendeleo ya maji
- Wanafunzi Kuripoti katika shule walizopangwa.Muhula wa kwanza kwa wanafunzi wa Kidato cha Tano kuanzia mwaka huu 2013 itaanza mwezi Julai. Wanafunzi wamepangwa katika shule zenye miundombinu na walimu kwa masomo husika. Aidha, kama baadae upungufu utajitokeza, wakuu wa shule wameelekezwa kufanya taratibu za kuazima walimu wa muda na kutoa taarifa kwa uongozi wa halmashauri husika kuhusu upungufu wa walimu uliopo.
Kwa nafasi hii, ninaagiza wanafunzi
wote kuripoti katika shule walizopangwa tarehe 29 Julai, 2013. Kama kutakuwa na sababu yoyote ya
msingi ya kuhamia shule nyingine, uhamisho wa kawaida utafanywa baada ya
kuripoti shuleni kupitia kwa mkuu wa shule husika, Mkurugenzi wa
Halmashuri/Manispaa na Katibu Tawala wa Mkoa. (Wizara haitabadilisha shule
walizopangwa wanafunzi)
- Wanaporipoti wanatakiwa kuwa na:Original Result slip na Living Cerificate