Sunday 31 March 2013

AIRTEL, UWF WALIPONIWEZESHA KUWA MWANAMAKUKA 2013


Nilipokuwa nakabidhiwa mfano wa hundi ya ushindi wangu namba mbili waTuzo za Mwanamakuka na Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde (kulia) Wanaoshuhudia kushoto ni  Mke wa Makamu wa Rais,  Asha Bilali na Mwenyekiti  wa Unit of Women Friends(UWF) Esther Wakati. picture 2 
Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde (kulia) akinikabidhi mfano wa hundi ya ushindi wangu wa pili wa Tuzo za Mwanamakuka 2013. Wanaoshuhudia (kulia katikati) ni Mwenyekiti  wa Unit of Women Friends (UWF) Esther (kushoto) Msimamizi wa tuzo hizo Mariam Shamo akifuatiwa na Mke wa Makamu wa Rais, Asha Bilal. picture 5 
Waandaaji na wadhamini wa Tuzo za Mwanamakuka 2013 wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mke wa Makamu wa Rais, Asha Bilali wakati wa sherehe za tuzo hizo zilizofanyika Machi 8, 2013.

TAASISI YA CATHERINE FOUNDATION DEVELOPMENT YATOA MISAADA  KWA WAGONJWA NA YATIMA JIJINI ARUSHA 

Taasisi ya Maendeleo isiyo ya kiserikali ya Catherine Foundation ya jijini Arusha leo imetoa misaada mbalimbali ya vyakula kwa wagonjwa Hospitali ya Mt Meru na vituo viwili vya Yatima vya Faraja na Lohada Moshono vyopte vya jijini humo.

Catherine Foundation Develeppent inaongozwa na Mbunge wa Viti Maalum UVCCM Arusha, Catherine Magigie.

Misaada hiyo ya vyakula na sabuni pamoja na kuwatembelea wagonjwa kufanyika ikiwa ni sehemu ya kuwapa faraja wagonjwa na yatima hao waki huu wa kuelekea siku kuu ya Pasaka ili nawao wajisikie ni miongoni mwa jamii.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akimkabidhi  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida Mokit msaada wa mablang’eti ya kujifunikia wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akiwajulia hali wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Mt. Meru ya jijini Arusha na kuwapa zawadi mbalimbali.
Ilikuwa ni uchungu sana kwa Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, alipopata taarifa za watoto zaidi ya 200 wanao lelewa katika kituo cha Yatima cha Faraja mjini Arusha. Watoto hao ni yatima ambao walitelekezwa na wazazi wao maeneo mbalimbali mjini humo na wengine ni waathirika wa Virusi vya Ukimwi. Mtoto aliyempakata alitupwa jalalani na wazazi wake angali mchanga na kulelewa hadi umri huo Hospitalini hapo.
Mbunge Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akimkabidhi  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida Mokit msaada wa vitu mbalimbali kwaajili ya wagonjwa waliolazwa Hospitalini hapo.
Wanachama wa CCM na Taaasisi ya Catherine Foundation Development inayoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum Arusha, Catherine Magige wakiwa wamebeba zawadi mbalimbali wakielekea katika moja ya wodi za akina mama na watoto Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha kukabidi zawadi hizo.
Mbunge Catherine Magige akiongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida Mokit wakifutana na wana Catherine  Foundation wakielekea kwenye moja ya wodi za wagonja hospitalini hapo kutoa misaada.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akiwa amewapakata watoto wawili mapacha waliozaliwa katika Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha.
 
 Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akisoma taarifa yake na kuzungumza na watu mbalimbali wakiwapo wafanyakazi wa Hospitali ya Mount Meru.
IMEHAMISHWA HABARI MSETO 

Airtel yachangia vitabu vya sayansi kwa shule tatu za Sekondari mkoani Mwanza

Meneja Huduma kwa wateja wa Airtel, Hawa Bayumi akimkabidhi msaada wa vitabu kwa Afisa Elimu wa mkoa wa Mwanza Hamisi Maulid kwa ajili ya shule tatu za sekondari za Kalebezo, Buhongwa na Kabuhoro zilizopo mkoani humo. Wanaoshuhudia (kulia) ni Meneja Mauzo wa Kanda, Ally Maswanya na Meneja Huduma ya Airtel Money wa Kanda, Galus Mgawe.
WAKATI Tanzania ikikabiliwa na uhaba wa wataalamu wa fani ya sayansi,wanafunzi wametakiwa kutohofia masomo ya sayansi na kukimbilia kusoma masomo mengine kwa lengo la kulifanya taifa liwe na wataalamu wengi wa fani mbalimbali.Kauli hiyo imetolewa jijini Mwanza na Afisa Elimu wa Mkoa wa Mwanza Hamis Maulid wakati akikabidhi vitabu kwa shule nne za sekondari za mkoa huo vilivyotelewa na kampuni ya simu za mkononi ya Airtel.

Afisa Elimu wa mkoa wa mwanza ameendelea kwa kusema elimu ni urithi endelevu na kusoma masomo ya sayansi kunamwezesha mwanafunzi kuwa katika nafasi nzuri ya kulisaidia taifa katika Nyanja ya kitaalamu. mataifa mengi duniani yamepiga hatua kutokana na wanafunzi kupewa msukumo wa kusoma masomo ya mchepuo wa sayansi.

Akiongea katika halfa ya makabithiano ya vitabu mkoani Mwanza, Meneja wa huduma kwa jamii wa kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Hawa Bayumi amesema Airtel imeguswa na tatizo la ukosefu wa vitabu mashuleni na kusababisha kiwango cha ufaulu kushuka hasa katika masomo ya sayansi. Na leo tunayofuraha kutoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari  za mkoa wa mwanza zikiwemo: Kalebezo  sekondari iliyopo wilayani Sengerema, shule ya sekondari ya Buhongwa na Kabuhoro sekondari.

Tunaamini mchango huu wa vitabu mashule utakuwa chachu ya maendeleo ya elimu nchini na kuongeza kiwango cha ufaulu nchini. Tunaahidi kuendelea kushirikiana na serikali chini ya wizara ya elimu katika kuhakikisha tunafikia malengo waliojiwekea. Aliongeza Bayumi.

 Naye Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Kalebezo iliyopo wilayani Sengerema Thomas Muswaga na mwanafuzi Julieth John wa kidato cha nne katika shule ya sekondari ya Buhongwa wanazungumzia changamoto mbalimbali zikiwemo uhaba wa vitabu na kushukuru Airtel kwa msaada wa vitabu walioutoa katika shule hizo za mkoa wa Mwanza.

Airtel chini ya mpango wake wa shule yetu imeendelea kutoa msaada wa vitabu kwa shule za sekondari mbalimbali nchini. kwa mwaka huu shule 93 za sekondari  tangu kuanzishwa kwa mradi huo shule zaidi  ya shule za sekondari 900 zimekabithiwa.

Tushirikiane kuinua sekta ya elimu nchini

Waziri wa Elimu na Ufundi Stadi, Dk Shukuru Kawambwa

MARA nyingi jamii imekuwa ikiinyoshea kidole serikali na kuwatupia lawama walimu  na wasimamizi wa elimu nchini kutokana na matokeo mabaya ya mitihani ya kitaifa.
Hata sasa mijadala inayoendelea mtaani ni juu ya matokeo yaliyotangazwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Mitihani, NECTA,yanayohusu mitihani ya kidato cha nne na cha pili, ambayo yamekuwa  na ufaulu mdogo kulinganisha na mwaka uliopita.
Kilichowachefua zaidi watu ni namna shule za serikali ambazo ni kilimbilio na tegemeo kwa wengi kwa miaka mingi, zimeanguka vibaya zikiachwa mbali na shule binafsi.
Yawezekana serikali inastahili lawama kwa kuwepo kwa matokeo hayo mabovu ya shule zake, pia kudidimia kwa kiwango cha elimu nchini kunakosababishwa na kushindwa kusimamia vema sekta hiyo kwa kuwatengenezea mazingira mazuri walimu.
Hakuna asiyejua kwa sasa nchini walimu wamekuwa ndio watumishi wa serikali dhalili kwa namna walivyosahauliwa wakicheleweshewa mishahara yao na malimbikizo ya pohso zao kiasi cha kuwavunja moyo wa kufundisha shuleni.
Leo walimu wamezigeuza shule wanazofundishia kuwa vijiwe vya kupiga soga na kuuza maandazi, ubuyu, kababu na karanga na kuwalazimisha wanafunzi kununua na kwenda na fedha za ziada shuleni kwa ajili ya masomo ya ziada.
Mtu unaweza kujiuliza mwalimu asiyeweza kumfundisha mtoto kwa muda wa kawaida wa masomo yaani saa 2 asubuhi hadi saa 8 mchana, anapataje muda wa kumsaidia mwanafunzi kwa masaa mawili ya masomo ya ziada?
Hata hivyo unabaini kuwa uwajibikaji mdogo na kukosa wito wa kazi ndio chanzo cha walimu wengi kuwa na 'mdadi' wa masomo ya ziada kwa vile unamuingizia pato nje ya pato lake halali la mshahara kama mtumishi wa serikali.
Hayo yote yanatokea siku hizi katika shule zetu kutokana na udhaifu ambao umekuwa ukionyeshwa na serikali na wasimamizi wa elimu katika kuhakikisha walimu wanalipwa fedha zao na kwa wakati pamoja na kupewa motisha mara kwa mara.
Licha ya kwamba uzembe huo unaofanywa na serikali katika usimamizi wa sekta ya elimu, bado jamii hususani wazazi na walezi nao wanapaswa kubeba mzigo wa lawama katika kuanguka kwa kiwango cha elimu nchini badala ya wenyewe kuwanyooshea wengine vidole.
Jamii kwa namna moja au nyingine ni sababu ya kuporomoka kwa kiwango cha elimu nchini kutokana na kutofuatilia kwa karibu maendeleo ya watoto wao wala kujua kama wanafika shuleni, wanasoma nini na wanafanya nini watokapo shuleni.
Nalisema hili nikirejea taarifa zilizotolewa na uongozi wa baraza la mitihani la taifa kwa mwaka wa pili mfululizo, baadhi ya watahiniwa na kidato cha nne kujibu maswali kwa kuandika na kuchora mambo machafu pamoja na kuandika nyimbo za Bongofleva.
Wanafunzi wanaofikia hatua ya kujibu au kuchora matusi kwenye karatasi za majibu ya mitihani yao, huenda hawana misingi mizuri ya malezi bora na wasiofuatiliwa na wazazi wao na hivyo kwenda shuelni sio kwa ajiliu ya kusoma bali kujifunza uhuni.
Kwa mwanafunzi mwenye kuachiwa hafanye atakalo bila kufuatiliwa na mzazi, hatma yake ni kwamba aingiapo kwenye mitihani huwa hana cha kujibu zaidi ya kuandika 'utumbo' kama huo wakiamini mradi wanamaliza mitihani yao na kupumzika.
Hapo ndipo mzazi anapolazikika kubeba mzigo wa lawama kwa matendo ya mtoto wa namna hiyo, naamini kama mzazi au mlezi ni mfuatiliaji wa maendeleo ya mwanae shuleni ni rahisi kugundua udhaifu wa mwanae na kumsaidia ikiwezekana 'kumnyoosha' kimaadili.
Lakini kwa vile wazazi wapo 'bize' kuhangaikia maisha na kusahau wajibu wao, ndio matokeo ya watoto hao kufanya madudu katika mitihani na matokoe yakitoka akiwa amefeli lawama zinaelekezwa kwa serikali na walimu wakati yeye mwenyewe ni chanzo.
Hivyo nilikuwa nawaasa wazazi na walezi, kuwa karibu na watoto wao na kufuatilia nyendo zao shuleni, kuwaacha watoto waishi kama kuku wa kienyeji bila kujua shuleni huenda kufanya nini, tutaendelea kushuka kwa kiwango cha elimu kila kukicha.
Ni kweli serikali wanapaswa kuboresha sekta ya elimu kadri iwezavyo, pia walimu kutekeleza wajibu wao ipasavyo, lakini wazazi na walezi hawapaswi kuwa watazamaji, wao wanapaswa kusimama kidete kuhakikisha mambo yananyooka kuanzia kwa watoto wao.
Kadhalika wanafunzi anapaswa kutambua wanapelekwa shuleni kujifunza na kusoma kwa faida yao, hivyo wakifuate kilichowapeleka na mambo ya kihuni na mengine ya kuiga ni kujiharibia mustakabali wa maisha yao ya baadae.
Kwa dunia ya sasa mtu bila elimu ni sawa na redio bila ya betri, waache kufanya ujinga na kuiga mambo ambayo hayana faida kwao hata kama wazazi na walezi wao hawafuatilii nyendo zao kwani mambo yanapoharibika hayawaharibikii wazazi au walezi wao bali wao wenyewe na siku zote majuto huwa mjukuu.

Sote tuwajibike kukomesha tatizo la mimba shuleni

Wanafunzi kama hawa wanapaswa kulindwa dhidi ya mimba wakiwa shuleni

TATIZO la mimba kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini, linachangia kurudisha nyuma maendeleo ya elimu.

Takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zinathibitisha kuwa tatizo hili limekuwa likiongezeka siku hadi siku hasa baada ya kuanzishwa shule za kata.


Pamoja na shule hizo kupunguza tatizo la wanafunzi kukosa nafasi za masomo, bado zinakabiliwa na changamoto nyingi.

Miongoni mwa changamoto hiyo ni tatizo la mimba kwa wanafunzi ambao wengi wao hulazimika kukatisha masomo, uhaba wa vifaa, vyumba vya madarasa, walimu na madawati.

Tafiti mbalimbali zimebaini kuwa, tatizo la mimba kwa wanafunzi hasa wa sekondari ni kubwa na linagusa hisia za kila mpenda maendeleo lakini jamii kubwa bado haijahamasika kutoa ushirikiano wa karibu kwa vyombo vya dola ili kuwafichua wahusika wa vitendo hivyo.

Baadhi ya wazazi hupokea rushwa kutoka kwa watuhumiwa ili wasifikishwe katika vyombo vya sheria na kuchukuliwa hatua stahiki ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia za aina hiyo.

Sisi tunasema dhamira yetu ni kuona jamii na wazazi wanashirikiana na vyombo hivyo kuhakikisha watuhumiwa wanakamatwa ili sheria iweze kuchukua mkondo wake.

Kama jamii itaona umuhimu huu, Tanzania yenye wasomi wazuri hasa kwa wanawake waliobobea katika fani mbalimbali itawezekana na maendeleo yatakuwa kwa haraka.

Kitendo cha jamii kuendelea kuwaficha wahusika wa vitendo hivi, kinarudisha nyuma juhudi za Serikali na wadau wa elimu kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu bora.

Imani yetu ni kwamba, uwajibikaji wa viongozi wa vyama na Serikali unahitajika kwa kuhamasisha jamii iboreshe maendeleo ya elimu hasa kwa mtoto wa kike na kukomesha tatizo la mimba.

Umefika wakati wa wanafunzi wetu, kupewa elimu ya kujitambua, kufahamu wajibu walionao kwa jamii na Taifa ili waweze kujithamini na kuepuka vishawishi vinavyoweza kusababisha wapate mimba au kuacha shule.

Nimalizie kwa kusema, elimu ni nyenzo muhimu kwa maendelo ya Taifa lolote Duniani kwani mapinduzi mengi ya maendeleo, hutegemea kiwango cha elimu kwa jamii husika. 
CHANZO:MAJIRA