TAASISI YA CATHERINE FOUNDATION DEVELOPMENT YATOA MISAADA KWA WAGONJWA NA YATIMA JIJINI ARUSHA
Taasisi ya
Maendeleo isiyo ya kiserikali ya Catherine Foundation ya jijini Arusha leo
imetoa misaada mbalimbali ya vyakula kwa wagonjwa Hospitali ya Mt Meru na vituo
viwili vya Yatima vya Faraja na Lohada Moshono vyopte vya jijini humo.
Catherine
Foundation Develeppent inaongozwa na Mbunge wa Viti Maalum UVCCM Arusha,
Catherine Magigie.
Misaada hiyo
ya vyakula na sabuni pamoja na kuwatembelea wagonjwa kufanyika ikiwa ni sehemu
ya kuwapa faraja wagonjwa na yatima hao waki huu wa kuelekea siku kuu ya Pasaka
ili nawao wajisikie ni miongoni mwa jamii.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige
ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akimkabidhi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida
Mokit msaada wa mablang’eti ya kujifunikia wagonjwa waliolazwa Hospitalini
hapo.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige
ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akiwajulia hali wagonjwa
waliolazwa Hospitali ya Mt. Meru ya jijini Arusha na kuwapa zawadi mbalimbali.
Ilikuwa ni uchungu sana kwa Mbunge wa
Viti Maalum, Catherine Magige ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine
Foundation, alipopata taarifa za watoto zaidi ya 200 wanao lelewa katika kituo
cha Yatima cha Faraja mjini Arusha. Watoto hao ni yatima ambao walitelekezwa na
wazazi wao maeneo mbalimbali mjini humo na wengine ni waathirika wa Virusi vya
Ukimwi. Mtoto aliyempakata alitupwa jalalani na wazazi wake angali mchanga na
kulelewa hadi umri huo Hospitalini hapo.
Mbunge Catherine Magige ambaye ni
Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akimkabidhi Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida
Mokit msaada wa vitu mbalimbali kwaajili ya wagonjwa waliolazwa Hospitalini
hapo.
Wanachama wa CCM na Taaasisi ya Catherine
Foundation Development inayoongozwa na Mbunge wa Viti Maalum Arusha, Catherine
Magige wakiwa wamebeba zawadi mbalimbali wakielekea katika moja ya wodi za
akina mama na watoto Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha kukabidi zawadi
hizo.
Mbunge
Catherine Magige akiongozana na Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Frida
Mokit wakifutana na wana Catherine Foundation wakielekea kwenye moja ya
wodi za wagonja hospitalini hapo kutoa misaada.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige
ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akiwa amewapakata watoto
wawili mapacha waliozaliwa katika Hospitali ya Mount Meru jijini Arusha.
Mbunge wa Viti Maalum, Catherine Magige
ambaye ni Kiongozi wa Taasisi ya Catherine Foundation, akisoma taarifa yake na
kuzungumza na watu mbalimbali wakiwapo wafanyakazi wa Hospitali ya Mount Meru.
IMEHAMISHWA HABARI MSETO
No comments:
Post a Comment