Monday, 17 March 2014

Wanawake msiwe tegemezi kwa kigezo cha kukosa ajiraWanawake hawapaswi kuwa wanyonge
 WANAWAKE wametakiwa kutokuwa tegemezi kwa kigezo cha kukosa ajira, badala yake wajiunge katika vikundi  vya ujasiriamali ili kujenga misingi  bora ya familia zao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam  juzi, Mratibu wa shirika lisilo la kiserikali Caritas linajihusisha na utoaji wa miradi  mbalimbali kwa kina mama, Glads Oning’o, alisema mwanamke ni nguzo ya familia, hivyo wajishughulishe ili kuzisaidia familia zao.
Alisema shirika hilo lina miradi ya kuwakopesha fedha kina mama  pamoja na mradi wa kilimo, ili waweze kujikomboa, kuondokana na hali tegemezi.

No comments:

Post a Comment