SOMKI - FURSA YA UDHAMINI KWA AJILI YA WANAFUNZI WA KIKE WENYE VIPAJI LAKINI HAWAJIWEZI
Tunayo furaha
kuwafahamisha kuwa kuna nafasi za udhamini kwa ajili ya wanafunzi wa kike wenye
vipaji lakini wasiojiweza, chini ya Mradi wa Somesha Mtoto wa Kike (SOMKI).
Mradi wa SOMKI unaleta utofauti katika maisha ya wanafunzi wa kike wa Tanzania
wanaoishi katika mazingira magumu na wasiojiweza na ambao wameonyesha vipaji
maalum au imeonekana kuwa na uwezo wa kufanya vizuri katika masomo yao na
kufikia viwango vya juu au daraja la kwanza katika mitihani yao.
Udhamini huu ni kwa
ajili ya kuhakikisha kwamba hawaathiriki na hali yao ya kimaisha ya sasa na
kwamba wanaweza kupata fursa ya kubadilisha maisha na kuwa na maisha bora.
Baada ya mchakato wa uhakiki na tathmini ya uhitaji itawapa walengwa fursa ya
kupata elimu na kuwapunguzia mazingira magumu wanayoishi na kujisomea.
Tunaelewa kuwa katika
shule yenu au utakuwa na taarifa kuwa kuna wanafunzi wanaostahili kupata nafasi
hii. Kwa barua hii tunaomba uweze kusambaza taarifa hii na kuhamasisha wale
wanaostahili kutuma maombi yao. Tafadhali nafasi hizi hutolewa mara moja tu kwa
mwaka. Maombi haya yako wazi hadi kufikia tarehe 30 Desemba 2013, kwa ajili ya
wanafunzi watakaodhaminiwa kitaaluma na Mradi wa SOMKI kwa mwaka 2014.
Maombi yatumwe kwenye
anuani iliyopo hapo chini. Na kwa maelezo zaidi msisite kututafuta kwa anuani
iliyopo hapo chini na namba ya simu.
Wenu mtiifu,
Jane M
Mratibu wa Mradi
No comments:
Post a Comment