Sunday, 3 November 2013

SOMA MATOKEO YA DARASA LA 7 YA MWANAO HAPA


Dar es salaam, Tanzania
MATOKEO ya Darasa la Saba yametangazwa  na mwaka huu huku ufaulu ukiwa umeongezeka kutoka asilimia 30.72 mwaka jana mpaka asilimia 50.61 mwaka huu kutokana na wanafunzi walio fanya mtihani mwaka huu wa darasa la saba wamefaulu zaidi ukilinganisha na wanafunzi wa mwaka jana Kaimu mtendaji wa Baraza la Mtihani Charles Msonda amesema ufaulu katika masomo yote umepanda kwa asilimia kati ya 6.01 na 28.06 ukilinganisha na mwaka 2012.
Mwaka huu watahiniwa wamefahulu zaidi katika somo la Kiswahili kwa asilimia 69.06 na somo walilio faulu kwa kiwango kidogo zaidi ni somo la Hisabati wamefaulu kwa asilimia 28.62.
 Msonda amesema jumla ya watahiniwa 427,606 kati ya 844,938 walio fanya mtihani huo wamepata alama ya 100 kati ya alama ya 250 idadi hiyo ni sawa na asilimia 50.61

No comments:

Post a Comment