Tuesday, 7 May 2013

BUDECO kujenga shule ya bweni kuwanusuru wanafunzi Busega

JUMUIYA ya Maendeleo ya Wanabusega (BUDECO) inatarajia kujenga shule ya bweni kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wanaokosa nafasi za kujiunga na sekondari za serikali katika jimbo la Busega.

Mwenyekiti wa jumuia hiyo, Ginhu Maselle, alibainisha hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa taarifa mbalimbali.

Alisema shule hiyo itakapokamilika itakuwa chini ya usimamizi wao lengo likiwa ni kuhakikisha wana Busega wanasonga mbele katika sekta ya elimu.

Aidha alikanusha madai kuwa jumuia hiyo imeingia katika mrengo wa kisiasa na kusisitiza kuwa jumuia hiyo ni kwa ajili ya maendeleo ya wana Busega bila kujali dini, rangi au kabila.

Naye Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo, ambaye pia ni mlezi wa jumuia hiyo, alisema yasiwekwe matarajio ya juu zaidi kwani yakiwekwa hayo na kushindwa kufanikiwa yatasababisha wakate tamaa ya kuendelea na kikundi.

No comments:

Post a Comment