|
Ama kweli watoto wakikalia madawati wanakuwa na furaha kabisa kama hawa |
|
Wakaamua kuchea na ngoma kabisa kushukuru |
Ukafika muda wa nasaha za tukio hilo
Blog hii inapongeza juhudi zifanywazo na Hassan Majaar Trust Fund
na tunaomba wadau kuisaidia taasisi hii
Na Mwandishi Maalum
Zaidi ya wanafunzi 750 katika shule saba
za wilaya ya Singida zitapokea msaada wa madawati yaliyotolewa kwa
ushirikiano kati ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust na Shirika La Nyumba
La Taifa
Jumla ya madawati 264 yanatolewa na wabia hao kupunguza tatizo sugu la upungu wa madawati katika shule hizo.
Hafla ya kukakabidhi madawati hao,
imefanyika katika Shule ya Msingi ya Munisa, iliyoko Halmashauri ya
Singida. Bwana Shariff Maajar, kwa niaba ya Taasisi ya Hassan Maajar
Trust akishirikiana na Bwana Nehemiah Mchechu kwa niaba ya Shirika La
Nyumba La Taifa, walikabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida
Dr. Parseko V Kone.
“Napenda kutoa shukurani za dhati
kwa Wakfu wa Hassan Maajar na Shirika La Nyumba La Taifa kwa msaada hu
mkubwa utakaochangia kuboresha elimu Singida’, alisema Dr. Kone.
Wanafunzi mkoani Singida, hususan,
walioko vijijini wanakabiliwa na changamoto kubwa la kwanza likuwa
mazingira ya kusomea, hivyo tunafarijika kuona wabia wanotusaidia
kuboresha mazingira ya elimu kwa watoto wetu. Hii inakuza viwango na
kuhimiza matokeo bora”, aliongeza.
Chini wa mradi wa Hassan Maajar
Trust wa “Dawati Kwa Kila Mtoto”, (A Desk For Every Child) mkoa wa
Singida wa pili kati ya mitano itakayonufaika kwa msaada inyaotelewa na
Hassan Maajar Trust kwa kutumia fedha zilizopatikana na michango
iliyotolewa kufwatia kampeni iliyoanzishwa Desemba 2011. Garama za
madawati haya ni Tsh 22,500,000, kati ya hizo Shirika La Nyumba La Taifa
limetoa jumla ya Tsh 10,000,000.
“Tunataka kuhakikisha kuwa kampeni
ya Dawati Kwa Kila Mtoto inawafikia watoto wengi iwezekenavyo na kujenga
maisha bora kwa watoto hao”, alisema Zena Tenga, Mkurugenzi Mtendaji.
“Tunashukuru Shirika La Nyumba La Taifa kwa kuunga mkono juhudi zetu.
Tutaendelea kuhamasisha ushirikiano na
wote wenye nia ya kuona lengo la Hassan Maajar Trust la kuhakikisha
watoto wetu wakiondoka sakafuni na kukaa kwenye madawati lina
timia”,aliongeza.
“Tunafurahi kuona kwamba mchango wa
shirika letu sasa uko katika hali ya madawati ambapo watoto watakaa na
watafurahia masomo ‘, alisema Bw. Mchechu, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika La
Nyumba La Taifa. , “ Shirika la Nyumba La Taifa lilishirikiana vema
na Taasisi ya Hassan Maajar Trust kuchangia fursa hii adimu kwa
wanafunzi na maendeleo ya elimu kwa ujumla”, aliongeza.
Kuhusu Hassan Maajar Trust
Taasisi
ya Hassan Maajar Trust imeandikishwa kama kampuni au NGO isiyo na hisa
na yenye kudhaminiwa na kufanya kazi za hisani bila faida. Lengo kuu la
Taasisi ya Hassan Maajar Trust ni kuboresha mazingira ya elimu katika
shule za Tanzania.
Kwa maelezo zaidi tembelea: www.hassanmaajartrust.org | www.hassanmaajartrust.blogspot.com
Kuhusu Shirika La Nyumba La Taifa
Malengo
ya Shirika la Nyumba la Taifa ni kuwa kampuni bora katika kuendeleza na
kusimamia ujenzi wa nyumba na majengo mengine yenye ubora kwa matumizi
ya umma. Ikifanya kazi katika misingi sahihi na imara ya kibiashara.
Kwa maelezo zaidi tembelea : www.nhctz.com
No comments:
Post a Comment