TAASISI ya kuhamasisha maendeleo na mawasiliano katika jamii yenye makao yake mjini Musoma mkoani Mara ya JAMII INFORMATION NETWORK inatarajia kufanya Kongamano kubwa litakalo wahusisha Wanafunzi zaidi ya 200 kutoka Shule 10 za Sekondari za Manispaa ya Musoma Mwezi Agosti mwaka huu, ikiwa ni njia ya kuhamasisha Maendeleo na uimarishaji wa Mawasiliano ndani ya Jamii.
Katika
Kongamano hilo mada mbalimbali zitatolewa na Wataalamu waliobobea
katika Masuala ya uhamasishaji wa Vijana Kupambana dhidi ya
Ukimwi,ujasiriamali,dhana ya kujiajiri,Changamoto katika Elimu kwa
Vijana pamoja na Ukatili wa Kijinsia ikiwa ni njia ya kujenga msingi bora wa makuzi kwa vijana wetu.
Mbali
na hivyo vijana hao pia wataelezwa jinsi ya kuwa Wazalendo katika nchi
yao,kupambana na rushwa,Umaskini lakini pia wakipata elimu sahihi ya
faida za uwekezaji kwa Tanzania,Sababu za Mimba za Mapema kwa watoto wa
kike na jinsi ya kujenga Mahusiano na Mawasiliano yaliyo sahihi.
Pamoja
na Mtandao huu kuwa na nia njema katika kuwasaidia vijana lakini bado
kumekuwepo na changamoto mbalimbali katika kufanikisha Kongamano hilo
hasa katika Suala la kifedha,hivyo basi Taasisi ya JAMII INFORMATION NETWORK kwa
nia njema inakuomba wewe Mtanzania,mpenda maendeleo,unaekaa ndani au
nje ya nchi,Mashirika kusaidia taasisi hii katika kufanikisha kongamano
hilo ili vijana wetu wakue katika makuzi mema na kujenga Tanzania ya
kesho iliyostaarabika.
Chanzo:Full Shangwe
No comments:
Post a Comment