Wanamakuka wenzangu, Aziza Mbogulume na Theonestina wakiwa makini kwenye semina hiyo ya Jumamosi |
Hawa ni baadhi ya jopo la waandaaji wa Tuzo ya Mwanamakuka. Wa pili toka kulia ni Bi. Mariam Shamo aliyetuwezesha kuhudhuria semina hiyo. |
Mimi na mshindi wa tatu wa tuzo za mwanamakuka Theonestina (kati) na mshindi wa kwanza Aziza Mbogulume (kulia) tukiwa katika pozi. |
JUMAMOSI mimi pamoja na Wanamakuka wenzangu tulioshinda mwaka huu wa 2013 tulikuwa miongoni mwa wanawake wajasiriamali tuliohudhuria mkutano na semina ya wajasiriamali iliyoandaliwa na kampuni ya Dare to Dream na kudhaminiwa na kampuni za Vodacom na Benki ya CRDB.
Ushiriki wetu katika semina hiyo iliyoambatana na maonyesho ya bidhaa za wajasiriamali wenzetu wa ndani na nje ya mkoa wa Dar uliwezeshwa na Mratibu wa Tuzo za Mwanamakuka, Bi. Mariam Shamo kutoka Umoja wa Wanawake Marafiki (UWF).
Kwa hakika tuliweza kujifunza vitu vingi ambavyo kabla ya semina na mkutano huo hatukuwa tunafahamu, hivyo mimi binafsi na kwa niaba ya wanamakuka wa 2013 tunamshukuru mno Bi Mariam na jopo zima la UWF, bila kuwasahau kampuni ya siku Airtel ambayo ilidhamini zawadi ya ushindi wangu wa pili.
No comments:
Post a Comment